TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kupitia kibali cha ajira
mpya chenye kumb. Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 chenye nafasi ya
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (4) na nafasi ya Dereva Daraja II (5) kutoka kwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu anatangaza nafasi za kazi na
anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo:
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II (NAFASI 04)
1.1.1 KAZI /MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri
ii. Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu
wake na ratiba za kazi zingine
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya
kazi
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu
husika
vi. Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six)
wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha,
wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa
dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel,
Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
1.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C1
2.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)
2.1.1 KAZI/MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari,
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
vi. Kufanya usafi wa gari: na
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake,
viii. Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
2.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja
(1) bila kusababisha ajali Pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya
kupata madaraja husika. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji
magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
2.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B1
TANGAZO LA KAZI NANYUMBU DC-DOWNLOAD HERE







Leave a Reply