NAFASI 23 ZA AJIRA MPYA KUTOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANG’ING’OMBE.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anatangaza nafasi za kazi zilizotokana na kibali cha ajira kipya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waombaji wenye sifa wanakaribishwa kuomba nafasi kama zilivyoainishwa hapa chini:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada ya Kazi | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|---|
| Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II | 4 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Stashahada (Diploma NTA Level 6) ya Masjala kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali- Ujuzi wa kompyuta | TGS C1 |
| Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II | 5 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Diploma ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6- Uwezo wa hatimkato maneno 100/min (Kiswahili & Kiingereza)- Ujuzi wa programu za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher) | TGS C1 |
| Dereva Daraja II | 13 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Leseni daraja E au C yenye uzoefu ≥ mwaka 1 bila kusababisha ajali- Cheti cha Basic Driving Course (VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali) | TGS B1 |
| Muhudumu wa Boti (Deckhand Auxiliaries) | 1 | – Elimu ya Kidato cha IV- Cheti cha Teknolojia ya Uvuvi (FETA) au Cheti cha Uhudumu wa Meli (DMI) au sifa inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali | TGOS A |
Masharti ya Jumla:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi 45.
- Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo wa maombi.
- Waambatishe wasifu binafsi (CV) yenye mawasiliano na majina ya wadhamini watatu.
- Vyeti vyote vya elimu na taaluma viwe vimeidhinishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya provisional results, statement of results na result slips (Form IV & VI) havikubaliki.
- Waombaji wa kada ya dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waombaji waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Vyeti vya nje ya nchi viwe vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET).
- Taarifa za kughushi hazitakubalika na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira:
https://portal.ajira.go.tz - DOWNLOAD HERE-TANGAZO LA KAZI WANGING’OMBE DC
Barua ya maombi ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
S.L.P. 64,
Njombe.
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Septemba, 2025





Leave a Reply