OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
15/10/2024
Kumb.Na.AB.113/388/01/25
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda
kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia
tarehe 23/10/2024 hadi 16/11/2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu
usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu
ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua
ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV,
VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na
sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji
ya tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti
vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili
namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
MWAJIRI: MDAS & LGAS
KADA: MWALIMU DARAJA LA III A – ELIMU YA AWALI
TAREHE YA USAILI WA MCHUJO:Oct. 23, 2024, 7 a.m.
MAHALI:
USAILI HUU UTAFANYIKA KATIKA VITUO MBALIMBALI KULINGANA NA ANUANI YA MUOMBAJI YA SASA (CURRENT
RESIDENT REGION) KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA TOVUTI YA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO:Nov. 16, 2024, 7 a.m.
MAHALI:
USAILI HUU UTAFANYIKA KATIKA MKOA AMBAO MSAILIWA ALICHAGUA NA KUTHIBITISHA KUWA AMEOMBA KAZI KATIKA
MKOA HUO. KITUO CHA USAILI UTAJULISHWA KUPITIA AKAUNTI YAKO YA AJIRA PORTAL NA TOVUTI YA SEKRETARIETI
YA AJIRA (www.ajira.go.tz).
See attachment Bellow.
20241510072349MWALIMU DARAJA LA IIIA -23-10-2024
Leave a Reply