Wakulima washauriwa kufuga bundi kudhibiti panya.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHA) umetoa wito kwa wananchi wa kuondoa imani potofu kuhusu ndege aina ya bundi na badala yake kuanza kuwafuga ili kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao wakiwemo panya.
Akizungumza kwenye Maonesho ya Nane Nane Ofisa kutoka TPHA, Mathias Benard amesema kisayansi bundi ni msaada mkubwa kwa wakulima kwa sababu hula panya na wadudu wengine wanaoathiri mazao.
“Bundi si wa kichawi, ni mlinzi wa mazao. Ana uwezo mkubwa wa kuona usiku, kusikia vizuri na kuwinda kimya kimya, hivyo ana uwezo wa kukamata panya bila kutumia sumu,” amesema.
Aidha, TPHA imeanza majaribio ya kufuga bundi kwa wakulima wachache katika Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo elimu hutolewa ya kutengeneza makasha ya kuwahifadhi ndege hao dhidi ya hatari.






Leave a Reply