Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026-Mhasibu (1) Apply now!

Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026-Mhasibu (1)  Baraza la Kiroho la Kitaaifa la Wabaha’i Tanzania

Baraza la Kiroho la Kitaaifa la Wabaha’i wa Tanzania (taasisi ya kidini) yenye makao makuu yake Makongo Juu, Dar es Salaam, inatafuta Mhasibu (1) mwenye sifa stahiki, uadilifu, sifa za kiroho na uzoefu wa kazi za uhasibu ili kujiunga na timu yetu ya fedha.
Nafasi hii inahitaji mtu mwenye uwezo wa kusimamia kwa ufanisi kumbukumbu za fedha, maandalizi ya taarifa za kifedha, na kuhakikisha uzingatiaji wa taratibu kanuni na viwango vya uhasibu vinavyotumika.

Majukumu ya Kazi Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026

  • Kuandaa na kutunza kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi
  • Kuandaa taarifa za kifedha za mwezi, robo mwaka, na mwaka
  • Kusimamia malipo na mapokezi ya fedha
  • Kufanya ulinganisho wa hesabu za benki (bank reconciliation)
  • Kusimamia bajeti na kufuatilia matumizi yake
  • Kuhakikisha uzingatiaji wa sera za fedha na kanuni za uhasibu
  • Kushirikiana na wakaguzi wa ndani na nje wakati wa ukaguzi wa hesabu
  • Kutunza nyaraka muhimu za kifedha kwa usalama na usiri
  • Kukagua uzingatiaji wa matakwa ya kisheria na kutoa ushauri ipasavyo
  • Kutetea mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya mkaguzi
  • Kuandaa malipo ya kisheria (NSSF, PPF, PAYE, SDL na WCF)
  • Kuandaa mishahara ya watumishi
  • Kukagua mifumo ya udhibiti wa ndani na kupendekeza maboresho
  • Kufanya ukaguzi wa ndani wa hesabu
  • Kuandaa uchambuzi wa madeni kwa umri (aging analysis) na kufuatilia madai ya fedha zilizotolewa (advances) ambazo hazijarudishwa
  • Kusaidia kujibu hoja na maswali kutoka kwa mkaguzi wa hesabu kitaalamu
  • Kusaidia kuendeleza mifumo itakayoongeza ufanisi wa ofisi ya fedha ya taifa
  • Kufuatilia taarifa za matumizi na stakabadhi za fedha zote zilizotolewa

Sifa za Mwombaji Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026

  • Shahada au Astashahada ya Uhasibu, Fedha, au taaluma inayohusiana
  • Awe na cheti cha kitaaluma kama CPA, ACCA, au sawa na hivyo
  • Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2 katika shughuli za uhasibu
  • Ujuzi mzuri wa matumizi ya mifumo ya uhasibu na programu za kompyuta (k.m. Excel, mfumo wa uhasibu)
  • Uwezo mzuri wa uchambuzi wa mwenendo na takwimu za kifedha

Ujuzi na Uwezo Binafsi Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026

  • Uwezo mzuri wa uongozi, na kufanya kazi na timu
  • Uwezo mzuri wa mawasiliano ya maandishi na ya mdomo
  • Uadilifu, uwajibikaji, na maadili mema ya kazi
  • Uwezo wa kufanya kazi bila shinikizo na kutatua changamoto kwa ufanisi
  • Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na kwa timu
  • Awe tayari kuwa eneo la kazi muda wote (full time) na kusafiri kama itakavyohitajika

Jinsi ya Kuomba Mhasibu Baraza la Wabaha’i Tanzania 2026

Waombaji wenye sifa watume barua ya maombi, wasifu binafsi (CV), nakala za vyeti na taarifa za Wadhamini, (nakala zote ziwe katika pdf file moja) kupitia barua pepe: secretariat@bahai.or.tz, kabla ya tarehe 10/07/2026.
Waombaji watakaochaguliwa ndio tutawasiliana nao kwa hatua zinazofuata.
Vodacom Tanzania Vacancies 2026
Vodacom Tanzania Vacancies 2026
GSM Group Vacancies 2026
GSM Group Vacancies 2026
Amana Bank Relationship Manager 2026
Amana Bank Relationship Manager 2026